Home » » Je, wajua? Je, wakumbuka?

Je, wajua? Je, wakumbuka?

Written By binally on Sunday, August 31, 2014 | 3:56 PM



Asalam alaykum…

Je, wajua? Je, wakumbuka?
…Nikujuze basi, nikukumbushe tafadhali.
Leo ni siku adhwimu, adimu tena muhimu. Ni siku ya kihistoria na historia tayari imejiandika. Tarehe 31.08.2013 ndiyo siku ambayo jumuiya ilizaliwa kisha baada ya siku kadhaa jina ikapewa. Tukumbuke ilianza kama Mubaarak Fund, kisha MYC na sasa rasmi ni MYIC.
Ni jambo zuri kukumbuka tulikotokea ili tuwe na mwanga wa kule tunakoelekea. Ni dhahiri shairi hakuna awezae kueleza wapi tunaelekea, ila ni rahisi sana kueleza wapi tumetokea.
Tulikuwa tunahesabu siku, wiki, miezi na sasa ni mwaka. Tunaamini utafika wakati tutahisabu miaka na kisha  miongo In shaa Allahla kujiuliza tumefanya nini katika kipindi cha mwaka mzima kuifanyia jumuiya?  kwa sababu mwisho wa yote haitajali tunamiaka mingapi ndani ya jumuiya, bali tumefanya mangapi kuifanyia jumuiya.


Hakika ni muda muwafaka wa kufanya tathmini katika kipindi cha mwaka mzima, wapi tumefanikiwa na wapi tumekosea? Mikakati gani ifanyike ili kurekebisha makosa yalojitokeza wakati uliopita?
Hakuna mwenye uwezo wa kurudi nyuma na kurekebisha makosa ya mwanzo ila kila mtu anaweza kuanza sasa kutengeneza mazuri ya baadae. Tukumbuke tarehe 1.09.2014 ni mwanzo wa mwaka mpya wa jumuiya hivyo lazima tuwe bora kuliko mwanzo tumepata nafasi nyingine. Hakika jitihada zilezile kawaida huleta matokeo yaleyale.
“Let us be better than before we got the second chance. The same efforts usually bring about the same results”
Umoja na mshikamano ndiyo malengo makuu ya jumuiaya yetu, “daima tushikamane katika kamba hii na wala tusifarakane”
Wapo ambao tulianza nao, mengi tukafanya nao, lakini sasa hatunao, Allah awalipe mema yao na pepo ndiyo iwe makazi yao.
Mwisho nawapa pole wote walofikwa na matatizo mbalimbali sambamba na kuwaombea dua. Pia nawapongeze wote walofaniksha mambo yao katika kipind cha mwaka mmoja wa jumuiya.
“Allah ilinde MYIC, Allah tuongoze wanaMYIC”


Imeandaliwa na Mohammed M. Ekome
Share this article :

+ comments + 2 comments

September 2, 2014 at 3:59 AM

May Allah guide our community and let us to be like a single body

September 3, 2014 at 4:32 AM

Allahumma amiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiin!

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Mubaarak Youth Islamic Community - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger