Home » , » FALSAFA YA MAISHA YA MUISLAMU II

FALSAFA YA MAISHA YA MUISLAMU II

Written By binally on Sunday, April 20, 2014 | 10:55 PM



NINATOKA WAPI?
                                                                              

Hili ni swali la pili la msingi. Watu wengi wamejaribu kutafuta jibu la swali hili, hata wengine wakabuni kuwa binadamu ametoka ghafla kwa bahati  nasibu. Mwaka 1971 Sharman M, mwandishi wa kitabu cha “Man, Civilization and Conquest” anasema “in the beginning 5000 million years ago, the Earth was spinning in space millions of years before there were any living plants or animals on it. 200 million years ago, there were plants, animals and birds on Earth millions of years before man appeared…..in 2 million years ago, there were also apes. Some of the apes after countless generations and more million years, became man-like….their brains become larger and their intelligent grew(uk 1) hii yaonesha kuwa hakukuwa na dalili ya uumbaji kwa fikra zao ila ni mabadiliko tu ya kimaumbile ambayo yalikuwa yakitokea baada ya miaka milioni kadhaa na tena baada ya milioni kadhaa tena mabdiliko mengine yanatokea hata kuja kupatikana kwa sokwe ambaye naye baada ya miaka milioni kadhaa akawa binadamu kamili.Hii ni sababu ambayo kimsingi haina msingi wa kiakili, kwa sababu ikiwa hata utando wa buibui hauwezi kutokea kwa bahati nasibu, iweje binadamu na mpango wake wa kimaumbile atokee kwa bahati nasibu?. Wengine wanasema kuwa mtu alianza kuwa nyani ndipo akabadilika taratibu hadi akawa mtu huyo ni Charles Darwin katika kitabu chake “The Origin Of Species”, na Sharman 1971, anasema “the gorillas and chimpanzees are put into our family tree because they are (our) remote COUSINS” yaani sokwe na nyani hawa ni ndugu zetu wa mbali.
                                                                             

Huu ni uongo ambao hadi leo unafundishwa mashuleni. Hata hivyo hadi leo manyani ni manyani na watu ni watu tu na hakuna kiumbe yeyote aliyewahi kuonekana sehemu yeyote duniani akiwa nusu mtu nusu nyani akiwa bado yupo katika hayo mabadiliko. Sisi waislamu tunasema hakuna binadamu atayeweza kutuambia sisi binadamu asili yetu nini au tunatoka wapi kinyume na anavyotueleza Yule alotuumba. Watu wote sisi  ni wageni katika hii dunia hivyo hivyo ni muhali kutokea mtu akajifanya mwenyeji sana kiasi cha kujua asili ya watu wakati yeye naye kajikuta katika duniani kama binadamu wengine. Hivyo mwenyezi mungu pekee ndio anayeweza kutuambia sisi tunatoka wapi na asili yetu ni nini, Allah anasema
 76:1
            “hakika ulimpitia binadamu katika dahali hakuwa ni mwenye kutajwa”(76:1) 
 Aya hii inatuambia kuwa kuna wakati tena mrefu tu ambapo mwanadamu hakuwapo kabisa, hivyo ni wazi kuwa alikuwa na mwanzo. Kuhusu mwanzo huu Allah anatuambia
 15:28
na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika hakika MIMI nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti,wenye kutokana na matope yaliyovunda!(15:28) 

Aya hii inatupasha habari ya kuumbwa kwa mtu baada ya muda mrefu kupita bila ya kuwepo dunia.Mtu aliumbwa kwa udongo, pengine mtu anaweza kubishia maelezo haya ya kuwa kaumbwa kwa udongo, maana inaweza kuwa vigumu kwake kulinganisha mwili wake unaowaka kwa mafuta na udongo. Lakini  kwa vile huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia, tunaweza kuhakikisha maneno ya mwenyezi mungu ni ya kweli pasi na shaka kwa kuangalia uhusiano wa udongo na mwili wa binadamu. Ukichunguza mwili wa binadamu utakuta una aina mbalimbali za madini kama vile chuma,calcium,phosphate,iodine n.k ambayo mtu hawezi kuyapata sehemu yeyote ila ARDHINI kwenye udongo,hivyo basi kuna uhusiano mkubwa kati ya mwili wa mtu na udongo .vilevile ukichunguza mahitaji ya mwili wa binadamu anahitaji vitu hivi kwa mahitaji ya mwili wake na vitu hivi vipo ardhini lakini kwa udhaifu wake hawezi kuvipata, Allah (sw) kwa rehma zake akamuumbia mimea na kisha ile mimea akaipa kazi, kwa kila mmoja kufyonza aina fulani pekee ya madini. Kwa mfano, muwa unafyonza sukari kutoka ardhini na kuhifadhi katika shina lake ili mtu aipate kiurahisi, wanga unafyonzwa kupitia ngano,mahindi,mpunga n.k, mafuta yanafyonzwa na ufuta,alizeti,karanga,minazi,pamba n.k na protini inafyonzwa na mimea yenye asili ya maharagwe kama vile kunde,mbaazi,maharagwe n.k vyote hivi vinafyonzwa kutoka ardhini/udongoni ili vitumike kujenga mwili uloumbwa kwa udongo hivyo ni lazima ujengwe kwa asili yake ambayo ni UDONGO
                                                                


Mwenyezi Mungu anatukumbusha kwa kusema
80:2480:25
 80:26

Hebu mtu na atazame chakula chake.Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu.Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. Kisha tukaotesha humo nafaka,Na zabibu, na mimea ya majani,Na mizaituni, na mitende, Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,Na matunda, na malisho ya wanyama; Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. (80:25-32)

Chakula ndicho kina mahitaji ya mwili hivyo Allah katika aya hii anatupa picha jinsi ya vyakula aina mbalimbali vinavyotokana na mimea ya aina mbalimbali inayoota baada ya kupasuliwa ardhi kuonesha jinsi gani mwili wa binadmu ulivyo na mahusiano na ardhi/udongo. Na katika kusisitiza hilo Allah anasema (55:14)

55:14
                                                       Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo
 Picha anayotupa Allah (SW) hapa ni kuwa mtu aliumbwa kama sanamu iliyofinyangwa(fakhaari)
Na kumbuka 15:28-29) "Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia."

Hapa tunapata habari kwamba baada ya Allah kumuumba mtu kwa udongo kama sanamu, akampulizia roho, akampa uhai, na ndipo mtu akawa mtu kama tunavyomfahamu, anaona, anasema, anasikia n.k

Hivyo tunamalizia jibu letu la asili ya mwanadamu kwa kusema Binadamu ana Asili mbili:
ü                Asili ya UDONGO, ambao ni asili ya kitu duni na
ü                Asili ya ROHO, ambayo ni asili ya kitu kitukufu sana.
                                                                                               itaendelea................
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Mubaarak Youth Islamic Community - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger