Kuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala amekuamrisha kuvaa Hijabu?
Mwenyezi Mungu anasema;
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)! Waambie wake zako, na binti
zako, na wanawake wa Kiisalamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea
upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.”
Al Ahzab = 59
Je! Mnazijuwa sifa za hijabu walokuwa wakivaa Masahaba wanawake
(RA)?
Anasema Aisha (RA);
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alikuwa akeshamaliza kusalisha sala
ya asubuhi (Alfajiri) wanawake huondoka wakiwa wamejifunika vitambaa vyao
hawajulikani kutokana na giza wala hawatambuani wenyewe kwa wenyewe.”
Bukhari na Muslim
Je unajuwa kuwa kuonyesha mapambo ni katika matendo ya wakati wa
ujahilia?
Mwenyezi Mungu anasema;
“Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama
walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili (zama za ujinga
– ukafiri).”
Al Ahzab – 33
Je unajuwa kuwa kujifananisha na makafiri kwa mavazi kunakufanya uwe
mfano wao?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Atakayejifananisha na kaumu yuko pamoja nao.”
Ahmed na Abu Daud – na hadithi
hii ni njema.
Je unajuwa kuwa Pepo imeharamishwa kwa wenye kuonyesha mapambo yao?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Aina mbili ni watu wa motoni sijapata kuwaona: Wanawake waliovaa
huku wakenda uchi, wanayumba wakiyumbisha, vichwa vyao mfano wa nundu la ngamia
lililoelemea upande mmoja. Hawatoingia Peponi wala hawataionja harufu yake.”
Muslim
Je unajuwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amewalani wanawake
wanaojifananisha na wanaume?
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amewalani wanaume wanaovaa nguo za
kike na wanawake wanaovaa nguo za kiume.”
Abu Daud na Ibni Majah na
hadithi hii ni sahihi.
Je unajuwa kuwa haijuzu kuvaa nguo nyepesi?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alisema kumwambia Osama bin Zeid;
“Mbona hujakivaa kile kitambaa kilichotoka Misri?”
Akasema;
“Nimempa mke wangu.”
Mtume (SAW) akamwambia;
“Mwambie avae shumizi
chini yake kwani naogopa isije
ikabainisha umbile lake.”
Ahmed na Al Baihaqiy na hii ni
hadithi njema
Je unajuwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) ameamrisha kuacha
kujipamba na kujipaka mafuta mazuri wakati wa kutoka?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Msiwazuwie wanawake kwenda misikitini, (lakini) watoke bila
kujipaka mafuta mazuri.”
Muslim
Je mnajuwa kuwa kujipaka mafuta mazuri mbele ya wanaume ni sawa na
kuzini?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Mwanamke yeyote atakayejipaka mafuta mazuri kisha akapita mbele ya
kundi wakaisikia harufu yake anakuwa keshafanya kitendo cha zina.”
Abu Daud – Attirmidhiy –
Annasai na hadithi hii ni sahihi
Je unajuwa kuwa mwanamke wa kiislamu hapigani vikumbo na wanaume?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alitoka msikiti akaona mchanganyiko wa
wanawaume na wanawake njiani.
Mtume (SAW) akasema;
“Jichelewesheni kwani haipasi kwenu kupita kati kati ya njia,
piteni kando ya njia.”
Wanawake wakawa wanakwenda wakijibana na ukuta hata nguo zao
zilikuwa zikiganda ukutani kutokana na kujibana kwao.
Abu Daud – hadithi njema
Post a Comment