MUHTASARI
MFUPI WA KIKAO CHA JUMUIYA
14/06/2015
MUBAARAK
CONFERENCE HALL
v
Kikao
kilifunguliwa kwa dua saa 10:52 jioni na wajumbe kukaribishwa kikaoni kisha
kutajwa ajenda za kikao.
AJENDA ZA KIKAO
* Mchakato wa
vitambulisho
* Usajili wa
jumuiya
* Akaunti ya jumuiya
* Uundaji wa
kamati kuu
* Mapato na
matumizi
* Mahudhurio
vikaoni
* Ushiriki katika
matukio ya wanajumuiya
* Miiko na maadili
* Mustakbali wa
jumuiya
* Mengineyo:
·
Bodi
ya wadhamini
·
Vyanzo
vya mapato n.k
v
Mchakato
wa Vitambulisho
Vitambulisho
tayari vilishakuwa katika mchakato wa kuvitoa na kilichopelekea kukwama ni
a.
technical
problem katika upande wa CAMERA, ambapo ziligoma kuonesha picha kwa upande
vitambulisho vya viongozi kwa camera zote mbili zilizotumika hivyo kukawa na
uzito.
b.
Kupiga
passport wakiwa na sare ya aina moja kwa akina dada ambapo zoezi hili
lilishindikana kufanyika ktk kikao cha tarehe 26/10/2014
Hata
hivyo zoezi bado lipo katika mchakato na kikao cha jumapili 21/06/2015
litafanyika zoezi la upigaji picha.
v
Usajili
wa jumuiya
Katika usajili
tulishindwa kutimiza baadhi viambatanisho muhimu ambavyo ni sehemu ya masharti
ya usajili na kutojua umuhimu wa kusajili jumuiya na faida zake,hivyo kupelekea
kusuasua kwa zoezi hilo. Hata hivyo kutokana na hali ilivyo hivi sasa ya kuwa
lazima tutambulike kwanza na taasisi fulan ndio tupate usajili, uongozi sasa
unalazimika kutafuta njia rahis na isokuwa na vikwazo ili kusajili jumuiya hii
ili kuepukana na urasimu uliopo.
v
Ufunguzi
wa akaunti
Mchakato tayari
ulishafanyika na kila kitu kilishakuwa tayari toka mwezi 11 mwaka jana juu ya
ufunguzi wa akaunti ambayo itakuwa na jina la jumuiya yaan MYIC Account. Zoezi
hili lilikwama baada ya kupata mkanganyiko wa taarifa;
a.
Mwanzo
tuliambiwa kufungua akaunti kuna hitaji majina ya viongoz wa 3, picha zao
pamoja na muhutasari wa kikao kinnacho ambatana na saini za wanajumuiya wote,
ila tulipo kamilisha hili tukaambiwa akaunti itakayofunguliwa ni joint venture
account amabyo haitakuwa na jina la jumuiya hivyo tukafeli.
b.
Sasa
ili kufungua account yenye jina la jumuiya ni lazima jumuiya isajiliwe nan do
utaratibu ambao umewekwa na wizara ya inayosimamia mashirika binafsi
inavyosemekana, kwa hiyo hili nalo tukafeli kwakuwa hatuna usajili.
Kinachofanyika
sasa ni ufuatiliaji ktk benki ya NMB tumedokezwa tunaweza kusajili bila ya usajili
hivyo tupo katika kufuatilia.
v
UUNDAJI
WA KAMATI KUU
Kutokana na
umuhimu wa kamati hii ilikuwa iwe tayari toka siku nyingi na ilikuwa ni moja ya
ajenda ktk kikao cha trh 26/10/2014 ila haikujadiliwa kiundani zaidi ya
kuongeza idadi ya wajumbe kutoka wa 3 mpaka wa5 ili kuleta uwiano sawa na idadi
ya viongoz ndan ya kamati hiyo ili yapatikane maamuz yasiyo na upendeleo. Hivyo
kikao cha leo kimefanikiwa kuwapata hao wajumbe watano waliopitishwa na
wanajumuiya wenyewe kwa hiari zao. Wajumbe hao ni;
1.
FAIDHA
MWANYEMBA
2.
KULTHUM
HASSAN
3.
MWANAKHATIBU
OMAR
4.
HUSSEIN
SENDARO
5.
HASSAN
WAZIRI
v
MENGINEYO
Kutokana na muda
ililazimika kujadili ajenda ya mengineyo ambapo mengi yalisemwa ;
A.
Kwann
sherehe ya Ibrahim Masoud ilisimamiwa na wana mubaark na si jumuiya?
JB:
tangu kupatikana kwa katibu, jumuiya haijihusishi na kuigharamia sherehe kwa
ujumla wake ila ni utoaji wa zawadi na cheti cha pongezi na vilifanyika, na
jumuiya pia ilikaa kikao trh 29/04/2015 kujadili uendeshaji wa hiyo sherehe
hivyo jumuiya ilishiriki.
B.
Nini
kimetokea kufanya jumuiya ifike hapa ilipofika?
JB:
yapo mengi yalotokea ila sasa ni wakati muafaka kwa viongozi kujibu hoja
kivitendo na kuacha blablah!
v
MAJUMUISHO
NA KUFUNGA KIKAO
a.
Kila
mwanajumuiya atatumiwa taarifa za madeni yake na atatakiwa kuonesha ushirikiano
katika hili
b.
Kamati
kuu itakutana ndani ya wiki hii ili kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya
jumuiya na wanachama
c.
Itatumika
orodha ya waliofika leo kuwapa taarifa kwa ajili ya kukutana jumapili ijayo kwa
kuendelea na jenda zilizobaki.
d.
mahudhurio
ya kikao kijacho ndo yatatumika kama
chujio la kuwachuja wasio kuwa active. Kutokuhudhuria ndio kujivua uanachama.
e.
Kikao
kimeahirishwa mpaka jpili saa 3:00 asubuhi
+ comments + 1 comments
Special thanks to our Secretary General for his clarification
May Allah give him strength to overcome all leadership challenges
Regards.
Post a Comment