Home » , » YALAITI NINGEJUA......!!! (soma kisa hiki )

YALAITI NINGEJUA......!!! (soma kisa hiki )

Written By binally on Monday, June 15, 2015 | 4:31 PM

Jamaa mmoja ambaye alikuwa ni fundi mjenzi,Aliajiriwa kwenye kampuni moja kubwa sana na kufanya kazi kwa muda mrefu sana huku akipata sifa mbali mbali kuhusu utendaji wake kuwa bora. Hakulewa sifa alizidisha utendaji wake na kufanya kampuni hiyo kupata tenda nyingi za ujenzi wa nyumba.
Alipofikisha umri wa utuuzima sana akaamua kuandika barua ya kustaafu kwenye kampuni hiyo.
Mmiliki wa kampuni alimjibu kwamba wameridhia kustaafu kwake lakini walimuamuru amalizie ujenzi wa nyumba moja ya ghorofa ya mwisho katika ujenzi wake. Alichukizwa sana na tendo hilo la kuongezewa kazi nyingine wakati yeye alikuwa anataka astaafu. 

Hivyo aliamua kuifanya kazi hiyo kwa roho upande na kuifanya ovyo...sehemu ya mchanga mwingi anatia simenti kidogo na sehemu ya simenti nyingi anatia maji mengi sehemu ya chuma anaweka mbao na sehemu ya mbao imara anaweka za kawaida..... Alifanya hivyo mpaka nyumba ikakamilika.... alipomaliza alifurahi sana na kusema hapa sasa nimewakomoa vya kutosha.
Aliwasiliana na mabosi wake na kuwaambia kwamba kazi yao imeisha cha ajabu aliambiwa kwamba ofisi nzima itakuja kuangalia kazi hiyo kisha ataruhusiwa rasmi kustaafu...kwa kuwa alishaamua na liwalo na liwe akaamua kujikaza na kuwasubiri.

Baada ya masaa machache mabosi pamoja na wafanya kazi wengine wa kampuni walifika na kuanza kumpongeza kwa kustaafu kwake kisha boss wake akamwambia hii ilikuwa ni surprise ya kampuni yao kwa utendaji wake bora ndani ya kampuni....Hivyo walikuja na hati za nyumba hiyo zikiwa na jina la jamaa pia wakamwambia funguo ulizonazo ni za kwako kutoka sasa hivyo wewe ni mmiliki halali wa nyumba hii na hii ni zawadi yetu kwako.
 
JAMAA AKAANZA KULIA NA KUSEMA HII NI KAZI YA MIKONO YANGU.... YALAITI NINGEJUA! NINGELIIJENGA KWA UFANISI NA UBORA WA HALI YA JUU!

je kama ungelikuwa wewe ungefanayaje??????????

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir R.A ambaye amesema: Mtume SAW amesema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia)).26

MAFUNZO TUNAYOPATA:
1. Kuwa na Hima ya kutenda mema na kubakia katika istiqaamah ili kitendo cha mwisho kabla ya kufariki kiwe ni kitendo chema, na kiwe ni kiliwazo siku ya kufufuliwa. [Al-Hijr 15: 99, Al-‘Imraan 3: 102].
((Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wakasemaSalaamunAlaykumamani iwe juu yenu. Ingieni Peponi kwa sababu ya yale [mema] mliyokuwa mkiyatenda)).

2. Umuhimu wa kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema) kabla ya kuaga dunia na sio kuwa katika maasi, khasa pale mtu anapofikia katika umri mkubwa.

3. Umuhimu wa kuomba du’aa ya Sunnah: ((Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik – Ee Allaah Mgeuza nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako))28, na Du’aa ya
Nabii Yuwsuf  (([Allaahumma] Anta Waliyyi fid-Duniya
wal-Aakhirah, Tawaffaniy Musliman wa-Alhiqniy bis-Swaalihiyn – Ee Allaah, Wewe ni Mlinzi wangu duniani na Aakhirah, Nifishie katika Uislamu na nikutanishe na waja Wema)), ili ajaaliwe mtu kuwa na
mwisho mwema kwani ((Allaah Huingia kati ya mtu na moyo)).

Ahsanteni.
Katibu~MYIC 2015.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Mubaarak Youth Islamic Community - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger