رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ [٢:١٢٧]
Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi [al-Baqarah 2:127]
رَبَّنَا
وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً
لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ
التَّوَّابُ الرَّحِيمُ [٢:١٢٨]
Ewe
Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni
mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za
ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu. [al-Baqarah 2:128]
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ [٢:٢٠١]
Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! [al-Baqarah 2:201]
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٥٠]
Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri [al-Baqarah 2:250]
رَبَّنَا
لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا
تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن
قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ
وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا
فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٨٦]
Mola
wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi!
Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola
wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na
uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya
makafiri [al-Baqarah 2:286]
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ [٣:٨]
Mola
wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe
rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji [Aal ‘Imraan 3:8]
رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ [٣:٣٨]
Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. [Aal ‘Imraan 3:38]
رَبَّنَا
اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ
أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٣:١٤٧]
Mola
wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo
yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya
makafiri. [Aal ‘Imraan 3:147]
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ [٧:٢٣]
Mola
wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu,
hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. [al-A’raaf 7:23]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [٧:٤٧]
Mola Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na madhalimu (watu walio dhulumu.) [al-A’raaf 7:47]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [١٠:٨٥]
Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. [Yoonus 10:85]
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [١٠:٨٦]
Na utuokoe kwa rehema yako kutokana watu makafiri. [Yoonus 10:86]
رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا [١٨:١٠]
Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu. [al-Kahf 18:10]
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ [١٤:٤٠]
Mola
wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu
pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. [Ibraaheem 14:40]
قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي [٢٠:٢٥]
وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي [٢٠:٢٦]
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي [٢٠:٢٧]
Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu
[Ta-Ha 20:25-27]
رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا [٢٠:١١٤]
Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu [Ta-Ha 20:114]
لَّا إِلَٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ [٢١:٨٧]
Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. [al-Anbiya’ 21:87]
رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ [٢٣:٢٩]
Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. [al-Mu’minoon 23:29]
رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ [٢٣:٩٧]
Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. [al-Mu’minoon 23:97]
وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ [٢٣:٩٨]
Mola wangu Mlezi, wasinikaribie. [al-Mu’minoon 23:98]
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ [٢٦:٨٣]
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. [al-Shu’ara’ 26:83]
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [٢٨:٢١]
Mola wangu Mlezi! Niokoe na watu madhaalimu. [al-Qasas 28:21]
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا [٢٥:٧٤]
Mola
wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na
utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu. [al-Furqaan 25:74]
رَبِّ
أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ
وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي
بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ [٢٧:١٩]
Ee
Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi
na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa
rehema yako katika waja wako wema. [al-Naml 27:19]
رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا [٢٥:٦٥]
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. [al-Furqaan 25:65]
Post a Comment