MAISHA YA MUISLAM
Mwanadamu katika maisha yake yote hana budi kufahamu ana
jukumu gani akiwa kama mwislamu katika dunia hii. Suala hili linakuja pale
mwislamu anapojitambua (self-actualization)
na kujitambua hakuwezekani mpaka mwislamu huyu ameweza kujibu maswali haya:-
Mimi ni nani?
Ninatoka wapi?
Niko wapi na kwanini?
Ninaelekea wapi?
Mwisho wangu utakuwa nini?
Haya ni ndio tunayoyaita maswali ya msingi. Mwislamu
anapoweza kujibu maswali haya na akazingatia majibu yake tunasema mtu huyo
amejitambua iliyobaki ni kutekeleza tu katika utendaji wa kitu chochote
kujitambua ndio jambo la msingi la kwanza kabisa. Kwa mfano: Meneja hawezi kuwa
meneja mzuri kama hajitambui kwa maana kwamba haelewi ilikuwa meneja mzuri
anatakiwa awe vipi na afanye mambo gani yanayomwajibikia, vivvyo hivyo muislamu
hawezi kuwa muislamu safi kama haelewi aweje na aishi vipi.
Katika Makala hii tutajaribu kutoa maelekezo ya majibu fasah
ya maswali haya ya msingi yanayomuwezesha muislam ajitambue na aishi kweli kama
muislamu.
MIMI NI NANI?
Mtu anapoulizwa wewe ni nani mara nyingi hukimbilia kutaja
jina lake. Kwa mfano: akasem mi ni kibabu, juma,zawadi,zainabu au kandoro.
Lakini ukweli ni kuwa yeye si kibabu, si juma, si zawadi au kandoro kwani hili
ni jina tu, kama ilivyo kwamba anashati,suruali, gauni na viatu.Sasa gauni,
shati, suruali na viatu ambavyo vyote ni vyake tukiviweka pembeni yeye anabaki
kuwa ni NANI? Kwa sababu kama ambavyo anaweza kubadilisha shati lake ,gauni au
suruali na vitu vingine na jina pia anaweza kubadilisha. Yeye ni kile kisichoweza kubadilika. Vilevile
anaweza kujibu mimi ni MTU. Bado jibu hili sio sahihi sana kwa vile hata UTU
anaweza asiwe nao pia akawa na tabia za kinyamatu.Hivyo utu pia hubadilika
hivyo mtu atatoa jibu fasaha na sahihi lisilo na utata kama atajibu mimi ni
KIUMBE. Mtu anapojitabulisha kwamba ni kiumbe ni wazi kuwa anatambua asili ya
kiumbe chochote kile ni kuumbwa na kukubali kwake kuwa kiumbe ni wazi kuwa
anakubali yeye kaumbwa. Na ili ajitambue vyema ni lazima afahamu kaumbwa na
nani. Hii ni wazi kwani hata mtoto mdogo hutambua kuwa amezaliwa na
anapojitambulisha vizuri humtaja baba yake. Kiumbe anayejitambulisha vyema
humjua muumba wake, SISI waislamu tunatambua muumba wetu ni MWENYEZI MUNGU (SW)
hata watu wengine ambao sio waislamu wanatambua kuwa yupo muumba ingawa
wanapuuzia ukweli huu au kumshirikisha.
NINATOKA WAPI?
itaendelea..........
Post a Comment