Definition List

.
Latest Post

YOU BETTER EAT IF YOU CAN'T...

Written By binally on Saturday, July 4, 2015 | 2:43 AM

ูˆَุนَู†ْู‡ُ ู‚َุงู„َ: ู‚َุงู„َ ุฑَุณُูˆู„ُ ุงَู„ู„َّู‡ِ ‏- ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู… ‏-{ ู…َู†ْ ู„َู…ْ ูŠَุฏَุนْ ู‚َูˆْู„َ ุงَู„ุฒُّูˆุฑِ ูˆَุงู„ْุนَู…َู„َ ุจِู‡ِ, ูˆَุงู„ْุฌَู‡ْู„َ, ูَู„َูŠْุณَ ู„ِู„َّู‡ِ ุญَุงุฌَุฉٌ ูِูŠ ุฃَู†ْ ูŠَุฏَุนَ ุทَุนَุงู…َู‡ُ ูˆَุดَุฑَุงุจَู‡ُ } ุฑَูˆَุงู‡ُ ุงَู„ْุจُุฎَุงุฑِูŠُّ, ูˆَุฃَุจُูˆ ุฏَุงูˆُุฏَ ูˆَุงู„ู„َّูْุธُ ู„َู‡ُ 1‏ .‏ ‏1 ‏- ุตุญูŠุญ.‏ ุฑูˆุงู‡ ุงู„ุจุฎุงุฑูŠ ( 6057 )‏، ูˆุฃุจูˆ ุฏุงูˆุฏ ( 2362 )‏، ูˆูˆู‡ู… ุงู„ุญุงูุธ ุฑุญู…ู‡ ุงู„ู„ู‡ ููŠ ู†ุณุจุฉ ู‡ุฐุง ุงู„ู„ูุธ ู„ุฃุจูŠ ุฏุงูˆุฏ ุฏูˆู† ุงู„ุจุฎุงุฑูŠ؛ ุฅุฐ ู‡ูˆ ู„ูุธ ุงู„ุจุฎุงุฑูŠ ุญุฑูุง ุญุฑูุง ุณูˆู‰ ุฃู†ู‡ ู‚ุงู„: " ุญุงุฌุฉ ุฃู† ูŠุฏุน " ุจุฏูˆู† " ููŠ " ูˆู„ุง ุฃุซุฑ ู„ุฐู„ูƒ.‏ ูˆุฃู…ุง ุฃุจูˆ ุฏุงูˆุฏ ูู„ูŠุณ ุนู†ุฏู‡: " ูˆุงู„ุฌู‡ู„ " ูˆู…ุง ุฃุธู† ุงู„ุญุงูุธ ุฐูƒุฑ ุฃุจุง ุฏุงูˆุฏ ูˆู„ุง ุนุฒู‡ ุฅู„ูŠู‡ ุฅู„ุง ู…ู† ุฃุฌู„ ู‡ุฐุง ุงู„ู„ูุธ.‏ ูˆุงู„ู„ู‡ ุฃุนู„ู….‏ Abu Hurairah (BAA) narrated that The Messenger of Allah (๏ทบ) said: “Whoever does not give up forged speech and evil actions and does not abandon foolishness, Allah is not in need of his leaving food and drink (i.e. Allah will not accept his FASTING).” Related by Al-Bukhari and Abu Dawud, and the wording is from the latter. Bulugh al-Maram English reference: Book 5, Hadith 684 (Fasting) Arabic reference: Book 5, Hadith 663

YALAITI NINGEJUA......!!! (soma kisa hiki )

Written By binally on Monday, June 15, 2015 | 4:31 PM

Jamaa mmoja ambaye alikuwa ni fundi mjenzi,Aliajiriwa kwenye kampuni moja kubwa sana na kufanya kazi kwa muda mrefu sana huku akipata sifa mbali mbali kuhusu utendaji wake kuwa bora. Hakulewa sifa alizidisha utendaji wake na kufanya kampuni hiyo kupata tenda nyingi za ujenzi wa nyumba.
Alipofikisha umri wa utuuzima sana akaamua kuandika barua ya kustaafu kwenye kampuni hiyo.
Mmiliki wa kampuni alimjibu kwamba wameridhia kustaafu kwake lakini walimuamuru amalizie ujenzi wa nyumba moja ya ghorofa ya mwisho katika ujenzi wake. Alichukizwa sana na tendo hilo la kuongezewa kazi nyingine wakati yeye alikuwa anataka astaafu. 

Hivyo aliamua kuifanya kazi hiyo kwa roho upande na kuifanya ovyo...sehemu ya mchanga mwingi anatia simenti kidogo na sehemu ya simenti nyingi anatia maji mengi sehemu ya chuma anaweka mbao na sehemu ya mbao imara anaweka za kawaida..... Alifanya hivyo mpaka nyumba ikakamilika.... alipomaliza alifurahi sana na kusema hapa sasa nimewakomoa vya kutosha.
Aliwasiliana na mabosi wake na kuwaambia kwamba kazi yao imeisha cha ajabu aliambiwa kwamba ofisi nzima itakuja kuangalia kazi hiyo kisha ataruhusiwa rasmi kustaafu...kwa kuwa alishaamua na liwalo na liwe akaamua kujikaza na kuwasubiri.

Baada ya masaa machache mabosi pamoja na wafanya kazi wengine wa kampuni walifika na kuanza kumpongeza kwa kustaafu kwake kisha boss wake akamwambia hii ilikuwa ni surprise ya kampuni yao kwa utendaji wake bora ndani ya kampuni....Hivyo walikuja na hati za nyumba hiyo zikiwa na jina la jamaa pia wakamwambia funguo ulizonazo ni za kwako kutoka sasa hivyo wewe ni mmiliki halali wa nyumba hii na hii ni zawadi yetu kwako.
 
JAMAA AKAANZA KULIA NA KUSEMA HII NI KAZI YA MIKONO YANGU.... YALAITI NINGEJUA! NINGELIIJENGA KWA UFANISI NA UBORA WA HALI YA JUU!

je kama ungelikuwa wewe ungefanayaje??????????

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir R.A ambaye amesema: Mtume SAW amesema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia)).26

MAFUNZO TUNAYOPATA:
1. Kuwa na Hima ya kutenda mema na kubakia katika istiqaamah ili kitendo cha mwisho kabla ya kufariki kiwe ni kitendo chema, na kiwe ni kiliwazo siku ya kufufuliwa. [Al-Hijr 15: 99, Al-‘Imraan 3: 102].
((Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wakasemaSalaamunAlaykumamani iwe juu yenu. Ingieni Peponi kwa sababu ya yale [mema] mliyokuwa mkiyatenda)).

2. Umuhimu wa kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema) kabla ya kuaga dunia na sio kuwa katika maasi, khasa pale mtu anapofikia katika umri mkubwa.

3. Umuhimu wa kuomba du’aa ya Sunnah: ((Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik – Ee Allaah Mgeuza nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako))28, na Du’aa ya
Nabii Yuwsuf  (([Allaahumma] Anta Waliyyi fid-Duniya
wal-Aakhirah, Tawaffaniy Musliman wa-Alhiqniy bis-Swaalihiyn – Ee Allaah, Wewe ni Mlinzi wangu duniani na Aakhirah, Nifishie katika Uislamu na nikutanishe na waja Wema)), ili ajaaliwe mtu kuwa na
mwisho mwema kwani ((Allaah Huingia kati ya mtu na moyo)).

Ahsanteni.
Katibu~MYIC 2015.

DONDOO FUPI ZA KIKAO CHA MYIC 14/06/2015

Written By binally on Sunday, June 14, 2015 | 4:13 PM



MUHTASARI MFUPI WA KIKAO CHA JUMUIYA
14/06/2015
MUBAARAK CONFERENCE HALL

v  Kikao kilifunguliwa kwa dua saa 10:52 jioni na wajumbe kukaribishwa kikaoni kisha kutajwa ajenda za kikao.

AJENDA ZA KIKAO
*  Mchakato wa vitambulisho
*  Usajili wa jumuiya
*  Akaunti ya jumuiya
*  Uundaji wa kamati kuu
*  Mapato na matumizi
*  Mahudhurio vikaoni
*  Ushiriki katika matukio ya wanajumuiya
*  Miiko na maadili
*  Mustakbali wa jumuiya
*  Mengineyo:
·         Bodi ya wadhamini
·         Vyanzo vya mapato n.k

v  Mchakato wa Vitambulisho
Vitambulisho tayari vilishakuwa katika mchakato wa kuvitoa na kilichopelekea kukwama ni
a.       technical problem katika upande wa CAMERA, ambapo ziligoma kuonesha picha kwa upande vitambulisho vya viongozi kwa camera zote mbili zilizotumika hivyo kukawa na uzito.
b.      Kupiga passport wakiwa na sare ya aina moja kwa akina dada ambapo zoezi hili lilishindikana kufanyika ktk kikao cha tarehe 26/10/2014
Hata hivyo zoezi bado lipo katika mchakato na kikao cha jumapili 21/06/2015 litafanyika zoezi la upigaji picha.

v  Usajili wa jumuiya
Katika usajili tulishindwa kutimiza baadhi viambatanisho muhimu ambavyo ni sehemu ya masharti ya usajili na kutojua umuhimu wa kusajili jumuiya na faida zake,hivyo kupelekea kusuasua kwa zoezi hilo. Hata hivyo kutokana na hali ilivyo hivi sasa ya kuwa lazima tutambulike kwanza na taasisi fulan ndio tupate usajili, uongozi sasa unalazimika kutafuta njia rahis na isokuwa na vikwazo ili kusajili jumuiya hii ili kuepukana na urasimu uliopo.

v  Ufunguzi wa akaunti
Mchakato tayari ulishafanyika na kila kitu kilishakuwa tayari toka mwezi 11 mwaka jana juu ya ufunguzi wa akaunti ambayo itakuwa na jina la jumuiya yaan MYIC Account. Zoezi hili lilikwama baada ya kupata mkanganyiko wa taarifa;
a.       Mwanzo tuliambiwa kufungua akaunti kuna hitaji majina ya viongoz wa 3, picha zao pamoja na muhutasari wa kikao kinnacho ambatana na saini za wanajumuiya wote, ila tulipo kamilisha hili tukaambiwa akaunti itakayofunguliwa ni joint venture account amabyo haitakuwa na jina la jumuiya hivyo tukafeli.
b.      Sasa ili kufungua account yenye jina la jumuiya ni lazima jumuiya isajiliwe nan do utaratibu ambao umewekwa na wizara ya inayosimamia mashirika binafsi inavyosemekana, kwa hiyo hili nalo tukafeli kwakuwa hatuna usajili.
Kinachofanyika sasa ni ufuatiliaji ktk benki ya NMB tumedokezwa tunaweza kusajili bila ya usajili hivyo tupo katika kufuatilia.


v  UUNDAJI WA KAMATI KUU
Kutokana na umuhimu wa kamati hii ilikuwa iwe tayari toka siku nyingi na ilikuwa ni moja ya ajenda ktk kikao cha trh 26/10/2014 ila haikujadiliwa kiundani zaidi ya kuongeza idadi ya wajumbe kutoka wa 3 mpaka wa5 ili kuleta uwiano sawa na idadi ya viongoz ndan ya kamati hiyo ili yapatikane maamuz yasiyo na upendeleo. Hivyo kikao cha leo kimefanikiwa kuwapata hao wajumbe watano waliopitishwa na wanajumuiya wenyewe kwa hiari zao. Wajumbe hao ni;
1.      FAIDHA MWANYEMBA
2.      KULTHUM HASSAN
3.      MWANAKHATIBU OMAR
4.      HUSSEIN SENDARO
5.      HASSAN WAZIRI

v  MENGINEYO
Kutokana na muda ililazimika kujadili ajenda ya mengineyo ambapo mengi yalisemwa ;
A.    Kwann sherehe ya Ibrahim Masoud ilisimamiwa na wana mubaark na si jumuiya?
JB: tangu kupatikana kwa katibu, jumuiya haijihusishi na kuigharamia sherehe kwa ujumla wake ila ni utoaji wa zawadi na cheti cha pongezi na vilifanyika, na jumuiya pia ilikaa kikao trh 29/04/2015 kujadili uendeshaji wa hiyo sherehe hivyo jumuiya ilishiriki.
B.     Nini kimetokea kufanya jumuiya ifike hapa ilipofika?
JB: yapo mengi yalotokea ila sasa ni wakati muafaka kwa viongozi kujibu hoja kivitendo na kuacha blablah!

v  MAJUMUISHO NA KUFUNGA KIKAO
a.       Kila mwanajumuiya atatumiwa taarifa za madeni yake na atatakiwa kuonesha ushirikiano katika hili
b.      Kamati kuu itakutana ndani ya wiki hii ili kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya jumuiya na wanachama
c.       Itatumika orodha ya waliofika leo kuwapa taarifa kwa ajili ya kukutana jumapili ijayo kwa kuendelea na jenda zilizobaki.
d.      mahudhurio ya kikao kijacho ndo yatatumika  kama chujio la kuwachuja wasio kuwa active. Kutokuhudhuria ndio kujivua uanachama.
e.       Kikao kimeahirishwa mpaka jpili saa 3:00 asubuhi

INNALILLAHI WAINNA ILAYHI RAAJIUUUN!

Written By binally on Monday, September 8, 2014 | 7:56 AM


Uongozi wa MYIC unasikitika kuwa tangazia wanajumuiya wote kuwa mwanajumuiya mwenzetu SALHA maarufu kwa jina la Dada TATIZO amefiwa na baba yake mzazi leo hii na yupo safarini kuja dodoma! hivyo shime aleykum wanajumuiya tujitokeze kwa wingi kumpa ushirikiano wetu dada yetu huyu katika kipindi hiki kigumu! hizi ni taarifa za mwanzo tu! taarifa kamili itawajia hapo baadae...........

Je, wajua? Je, wakumbuka?

Written By binally on Sunday, August 31, 2014 | 3:56 PM



Asalam alaykum…

Je, wajua? Je, wakumbuka?
…Nikujuze basi, nikukumbushe tafadhali.
Leo ni siku adhwimu, adimu tena muhimu. Ni siku ya kihistoria na historia tayari imejiandika. Tarehe 31.08.2013 ndiyo siku ambayo jumuiya ilizaliwa kisha baada ya siku kadhaa jina ikapewa. Tukumbuke ilianza kama Mubaarak Fund, kisha MYC na sasa rasmi ni MYIC.
Ni jambo zuri kukumbuka tulikotokea ili tuwe na mwanga wa kule tunakoelekea. Ni dhahiri shairi hakuna awezae kueleza wapi tunaelekea, ila ni rahisi sana kueleza wapi tumetokea.
Tulikuwa tunahesabu siku, wiki, miezi na sasa ni mwaka. Tunaamini utafika wakati tutahisabu miaka na kisha  miongo In shaa Allahla kujiuliza tumefanya nini katika kipindi cha mwaka mzima kuifanyia jumuiya?  kwa sababu mwisho wa yote haitajali tunamiaka mingapi ndani ya jumuiya, bali tumefanya mangapi kuifanyia jumuiya.


Hakika ni muda muwafaka wa kufanya tathmini katika kipindi cha mwaka mzima, wapi tumefanikiwa na wapi tumekosea? Mikakati gani ifanyike ili kurekebisha makosa yalojitokeza wakati uliopita?
Hakuna mwenye uwezo wa kurudi nyuma na kurekebisha makosa ya mwanzo ila kila mtu anaweza kuanza sasa kutengeneza mazuri ya baadae. Tukumbuke tarehe 1.09.2014 ni mwanzo wa mwaka mpya wa jumuiya hivyo lazima tuwe bora kuliko mwanzo tumepata nafasi nyingine. Hakika jitihada zilezile kawaida huleta matokeo yaleyale.
“Let us be better than before we got the second chance. The same efforts usually bring about the same results”
Umoja na mshikamano ndiyo malengo makuu ya jumuiaya yetu, “daima tushikamane katika kamba hii na wala tusifarakane”
Wapo ambao tulianza nao, mengi tukafanya nao, lakini sasa hatunao, Allah awalipe mema yao na pepo ndiyo iwe makazi yao.
Mwisho nawapa pole wote walofikwa na matatizo mbalimbali sambamba na kuwaombea dua. Pia nawapongeze wote walofaniksha mambo yao katika kipind cha mwaka mmoja wa jumuiya.
“Allah ilinde MYIC, Allah tuongoze wanaMYIC”


Imeandaliwa na Mohammed M. Ekome

sherehe ya kharusi Ramadhan Mwanangwa na Hawa Mustafa

Written By binally on Monday, June 16, 2014 | 10:10 AM

mashaallah

Written By binally on Wednesday, May 14, 2014 | 12:38 PM


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Mubaarak Youth Islamic Community - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger